Accessibility Settings

color options

monochrome muted color dark

reading tools

isolation ruler

Ripoti

Vifaa Vya Kutafitia Mtandaoni

Kwa muda mrefu, vifaa vya kutafitia mtandaoni na mbinu za upekuzi zilizotayarishwa na mpekuzi mbobezi wa mtandaoni wa shirika la BBC Paul Myers zimekuwa chanzo cha kutafiti mtandaoni kwa wasomaji wa GIJN. Tovuti yake, Kliniki ya Utafiti, ina ukwasi wa linki za kutafitia na “nyenzo za kujifunzia.” Hivi hapa vidokezi kuhusu jinsi ya kuwatafuta watu mtandaoni ambavyo Myers aliwasilisha kwenye mkutano wa GIJN wa mtandaoni wa mwaka 2019. Pia kuna makala ya GIJN ya maandishi kuhusu wasilisho la Myers kwenye GIJC19, kwa jina Maswali Manne kwa Mpekuzi Mbobezi wa Mtandaoni Paul Myers.

Tazama pia miongozo mingine ya Myers kwenye gijn.org:

Jinsi ya Kutumia Twitter Kutafuta Watu Kwenye Eneo la Tukio la Habari Inayoendelea Kutukia

Badilisha Kivinjari: Kutumia Vifaa vya Nyongeza Kwa Utafiti Kwenye Wavuti

Vifaa vya Nyongeza Kwenye Kivinjari (Sehemu ya 2): Kurejea Nyuma Kiwakati

GIJN’s Investigative Toolbox, ambayo ni makala ya Alastair Otter wa GIJN inaangazia mada lengwa:

Kufuatilia Majina na Tovuti, Kuhakiki Video, Mashine ya Utafutaji Jumuishi

Kuchimbua Habari za Watu, Utafutaji wa Kina Wavutini na Kujiweka Salama

Kutafuta Usuli wa Watu na Kampuni

Kuchimbua Twitter na Kufuatilia Sasisho za Tovuti

Zaidi ya Lahajedwali na Utafutaji wa Kina Wavutini

Jake Creps hutoa mtiririko dhabiti wa vidokezi muhimu kwenye blogu yake. Vile vile yeye huwa mwalishi wa podikasti, osintpodcast.com. Creps ni mchanganuzi wa data zinazokusanywa hadharani ili zitumike katika muktadha angavu, na ana uzoefu katika sekta za umma na binafsi.

OSINTcurio.us hujumuisha podikasti za kila wiki, matangazo ya mtandaoni na “vidokezi kwa dakika 10” kwa video vinavyoangazia vipengele kadha vya kufanya upekuzi kwa kutumia vyanzo vya hadharani. Ni mradi wa kijamii ulioanzishwa mwakani 2018 na wataalamu wachangiaji 10.

Sector035, inayojiita “Mbobezi asiyefahamika alivyo,” hutoa vidokezi mbalimbali kila wiki, hasa kuhusu utambuzi wa mahali fulani kwa kutumia mbinu mbalimbali za data. Huchapisha katika Week in OSINT na Quiztime.

Online Methods to Investigate the Who, Where, and When of a PersonHii ni orodha nyingine murua ya mtaalamu wa utafutaji kwenye intaneti Henk Van Ess. Tazama pia Who Posted What, “kiungo cha Facebook cha kutafutia maneno makuu ambacho kwacho waweza ukafatuta machapisho kwenye Faceboook yaliyo na neno kuu, katika tarehe fulani au baina ya tarehe mbili.” Hili ni wazo la Van Ess lililokuzwa na Daniel Endresz.

The Open Source Intelligence Framework ina orodha ya kina na inayokua kila wakati kuhusu vifaa vya kuchunguzia vya kidijitali.

Searching the Deep Web, na Giannina Segnini. Wasilisho hili linaloanza kwa vidokezi vya ujuzi wa hali ya juu kuhusu utafutaji wa Google wenye ustadi mkubwa liliwasilishwa kwenye kongamano la GIJC17 na mkurugenzi wa Uanahabari wa Data katika Columbia University Journalism School. Linaangazia matumizi ya Google kama daraja la kufanya utafiti wa kina likitumia ulanguzi wa dawa kama mfano. Linajadili ufuatiliaji wa kontena, meli, na bandarini. Pia, linaangazia utafiti kwenye Facebook na kadhalika.

How to Become a Deep Web Super Sleuth. Makala hii ya GIJN inaelezea mashauri yaliyotolewa na Albrecht Ude, mwanahabari wa Ujerumani, mtafiti na mkufunzi kwenye Kongamano la 11 la Uanahabari wa Upekuzi wa Kimataifa. “Mashine za utafutaji ni bure kabisa katika kutafuta chochote kwenye wavuti wa kina,” alisema Ude, ambaye ushauri wake wa kwanza ulikuwa kuwaza kidhahania, ikifuatiwa na vidokezi zaidi. Tazama pia jarida linalohusiana: Kutafuta na kutumia hifadhidata. 

Utafutaji Kwa Google Wa Kina Zaidi

Tumia ukurasa wa Utafutaji wa Kina Zaidi kwa Google, na maelezo yao kuhusu utafutaji wa kina zaidi. Google pia wanatoa mafunzo kwa wanahabari, likiwemo somo la utafutaji, ambayo ni kozi ya “utafutaji wenye uwezo”, na kadhalika.

Kwa kupata orodha ya amri za msingi tazama Sintaksia ya Utafutaji wa Google kwa Kina na Paul Myers.

Kwa maelezo ya msingi, tazama Vidokezi vya Utafutaji wa Google kwa Wanahabari na ExpertiseFinder

Utokapo hapo, jaribu:

Kazi za Daniel Russell Search Research na Google Advanced Search Operators.

37 Advanced Google Search Tips for Smarter Searching kutoka kwa Eric Melillo wa COFORGE.

Google Advanced Search: Tips and Operators for Better Searches na David Vranicar wa Oberlo.

Google Advanced Search: How to Find Better Info (2X Faster) kutoka Keyword Tool Blog.

Google Search Operators: The Complete List (42 Advanced Operators) na Joshua Hardwick akiwa ahrefsbog.

Advanced Google Search kutoka maktaba ya Chuo Kikuu cha Texas San Antonio.

OSINT Essentials na Eoghan Sweeney unatoa linki kwa vifaa na huduma zisizo na malipo ambazo ni muhimu kwa uhakiki wa mtandaoni, uanahabari wa kidijitali, na kazi ya upekuzi wa vyanzo vya hadharani.

First Draft, ni shirika lisilo la faida ambalo huwasaidia wanahabari na hujumuisha mambo mengi katika zana yake Advanced Toolkit. Tazama pia Mwongozo muhimu wa First Draft wa Kuhakiki Habari za Mtandaoni (PDF) (2019) na nyenzo za kufunzia zinazohusiana.

Tools, Useful Links & Resources, na Raymond Joseph, mwanahabari na mkufunzi katika shirika la Southern Tip Media nchini Afrika Kusini. Inajumuisha kurasa sita za habari juu ya Twitter, mitandao ya kijamii, uhakiki, habari kuhusu kikoa na anwani za IP, vitabu vya anwani vya kimataifa, na kadhalika. Katika wasilisho linalohusiana la GICJ17, Joseph alielezea “Jinsi ya kuwa Mpelelezi wa Kidijitali.” 

Exposing the Invisible ina miongozo mbalimbali kwenye tovuti yake, ikiwemo kuhusu “googleDorking,” mbinu ya kutafutia mashine za ufatutaji habari zilizofichwa kwenye tovuti za umma na mapungufu yaliyodhihirishwa na seva za umma. Miongozo mingine inaangazia utafutaji wa metadata na kutumia WHOIS.

Knowing Your Way Around The Command Line, na Max Harlow, Msanidi Programu Mwandamizi wa Chumba cha Habari katika The Financial Times, iliwasilishwa katika GIJC19. Nini chawezekana? Anatoa muhtasari: Tafuta anayemiliki tovuti, changanua data kwa upesi sana, linganisha majina yaliyoandikwa tofauti, unganisha data yako kwa hifadhidata zilizo mtandaoni, fanya utafutaji jumla kwenye mamia ya stakabadhi.

AML RightSource, shirika la binafsi nchini Marekani “linalojishughulisha pekee na vita dhidi ya ulanguzi wa fedha (AML)/Kipengee cha Sheria ya Siri za Benki (BSA) na utii kwa suluhu za uhalifu wa kifedha,” waliweka pamoja mkusanyiko wa rasilimali.

Investigate with Document Cloud, na Doug Haddix, Mkurugenzi Mkuu wa Investigative Reporters and Editors. Ni mwongozo wa kutumia stakabadhi za umma milioni 1.6 zilizotolewa na wanahabari, ukichanganua na kuonesha stakabadhi zako, kushirikiana na wengine, kusimamia usambazaji wa stakabadhi, na kusambaza kazi yako mtandaoni.

Malachy Browne’s Toolkit. Inahusisha zaidi ya linki 80 zinazoelekeza kwenye vifaa vya upekuzi wa vyanzo vya hadharani vilivyoundwa na mmoja wa wabobezi katika tasnia hii. Wakati produsa mwandamizi wa makala ya New York Times alionesha slaidi hii alipohitimisha kipindi chake katika GIJC17, karibu kila mtu aliomba kuipata.

An Investigative Guide to LinkedIn uliundiwa Bellingcat na Nathan Patin mwaka 2019. “Mwongozo huu unalenga kutoa vifaa muhimu na mbinu za kutambua wasifu wa watu kwenye LinkedIn na kudondoa taarifa ambazo zitakuwezesha kuelekea kwenye wasifu wa mlengwa kwenye mitandao ya kijamii.”

A Guide to Open Source Intelligence (OSINT) na Michael Edison Hayden kwa niaba

ya Tow Center for Digital Journalism katika Columbia Graduate School Journalism School (2019) inaangazia mada mbalimbali:

  • Tofauti baina ya mitandao iliyo wazi na iliyofungwa.
  • Utafutaji kwenye wavuti wazi
  • Kuhakiki uhalisia wa akaunti za mitandao ya kijamii
  • Kuhakiki picha na video
  • Kuchunguza tovuti za mitandao ya kijamii
  • Kutumia Majalada, Kuhifadhi Kazi Yako
  • Kujifunza Majukwaa Mapya na Kuingiliani na Jamii Kali

Finding Former Employees, na James Mintz. “Vidokezi 10 juu ya Uanahabari wa Upekuzi Kuhusu Hatua Yenye Nguvu Zaidi: Kuwasiliana na Wafanyakazi wa Zamani,” kulingana na mpelelezi gwiji wa kibinafsi Mintz, ambaye pia ni mwasisi na rais wa The Mintz Group.

Tools and tips for digging into Facebook from two investigative journalists Mahojiano ya mwaka 2019 na Brooke Williams, mwanahabari mpekuzi aliyewahi kutuzwa na ambaye pia ni mhadhili msaidizi wa Mazoezi ya Uanahabari Utumiao Kompyuta na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Boston, na  Henk van Ess, mpekuzi mwandamizi katika Bellingcat.com.

Investigative Research Links kutoka kwa mhariri wa utafiti Margot Williams unatoa mapendekezo kadha, tokea “Utafutaji Kwa Google Wenye Ufanisi” hadi kwa orodha ya tovuti za “Watafiti Waliobobea. Tazama pia jarida lake la GIJC19: Research Plan for Investigative Project.

Bellingcat’s Online Investigative Toolkit  inajumuisha rasilimali kadha kuhusu ramani, utafutaji unaojikita kwenye utambuzi wa mahali, picha, mitandao ya kijamii, usafiri, taswira ya data, wataalamu, na kadhalika.

Bureau Local collaborative tools ni mkusanyiko wa lahajedwali ya zaidi ya orodha 80, baadhi yazo ni vifaa vya kutafitia, vilivyofadhiliwa na Bureau of Investigative Journalism ya Uingereza.

Tools for Reporters na Samantha Sunne, hutoa barua pepe za mara kwa mara kuhusu ujuzi mpya, kama vile Kutafuta barua pepe wakati hazitaki kupatikana.

Fundamental search for journalists mfululizo wa mafunzo haya ya mtandaoni kutoka Datajournalism.com, yafundishwayo na Vincent Ryan, yanaangazia utafutaji wa kina, uhakiki, taswira na uundaji wa ramani kwa kutumia teknolojia ya utambuzi wa mahali.

SPJ Journalist’s Toolbox kutoka kwa Society of Professional Journalists nchini Marekani, iliyokusanywa na Mike Reilley. Inajumuisha orodha ndefu ya vifaa.

IntelTechniques ni tovuti iliyoundwa na Michael Bazzell, mpekuzi wa zamani wa uhalifu wa kompyuta aliyefanya kazi na serikali ya Marekani, ambaye sasa ni mwandishi na mkufunzi. Tovuti hiyo hupakia podikasti yake kwa jina The Privacy, Security, & OSINT Show.

How to find an academic research paper, na David Trilling, mwandishi wa Journalist’s Resource, iliyoko kwenye kituo cha Shorenstein Center on Media, Politics and Public Policy cha Harvard.

World.192.com ina orodha ya nambari za simu za kimataifa.

Using Phone Contact Book Apps For Digital Research, ni nakala elekezi ya mwaka 2019 iliyoandikwa na Aric Toler wa Bellingcat.

Use Chrome Developer Tools to View Masked Phone Numbers for Free on a Popular People Search Site, na Sean Lawson, profesa wa Chuo Kikuu cha Utah, iliyochapishwa mwaka 2019.

Using deep web search engines for academic and scholarly research, nakala ya Chris Stobing katika VPN & Privacy, chapisho la Comparitech.com, kampuni ya Uingereza inayolenga kuwasaidia watumiaji wafanye maamuzi mwafaka wanapojisajili kwa huduma za teknolojia kama vile VPN.

Step by step guide to safely accessing the darknet and deep web, an article na Paul Bischoff katika VPN & Privacy, chapisho la Comparitech.com, kampuni ya Uingereza inayolenga kuwasaidia watumiaji wafanye maamuzi mwafaka wanapojisajili kwa huduma za teknolojia kama vile VPN.

Research Beyond Google: 56 Authoritative, Invisible, and Comprehensive Resources, rasilimali kutoka kwa Open Education Database, shirika la Marekani litoalo mpangilio wa elimu ya kina ya mtandaoni wenye chaguzi za kujifunza bila malipo na kwa kulipia.

The Engine Room, shirika lisilo la serikali nchini Marekani liliunda Utangulizi kwa Rasilimali za Wavuti, inayojumuisha sehemu ya kurudufu nakala za habari ili kuzilinda zisipotee au kubadilishwa.

Awesome Public Datasets, mkusanyiko mkubwa uliojengwa na jamii na uliopangwa kwa mada.

Resources from Startme.com Mkusanyiko wa rasilimali nyingi kutoka kwa kampuni iliyotengeneza hifadhi ya alamisho jumuishi. Maktaba hii isiyo ya malipo ina kurasa zilizo na mamia ya linki:

Vifaa ya Kuongeza
Hifadhidata
Mashine za Utafutaji
Vifaa
Zana ya Vifaa vya Uhakiki
Miongozo

Hifadhidata, kwa mfano, ni ukurasa wenye linki za nyenzo mbalimbali kama vile mali zilizoibwa, hali ya hewa, usafiri, uchanganuo, usajili wa kikoa, majengo, wanyama, ndege zisizo na rubani, fedha na kadhalika.

Bates InfoTipsna Mary Ellen Bates, ni chanzo chema cha mawazo ya kisasa kama vile udhibiti wa matokeo ya Google News kwa kutumia kipindi cha wakati fulani na kutafuta watu kupitia utafutaji kwa jedwali la Facebook. Bates ni “mwasisi na msimamizi mkuu wa Bates Information Services Inc. na mtaalamu wa habari wa muda mrefu.”

Research Buzz iliandika Going Old School to Solve A Google Search Problem kuelezea mbinu ya kutenga baadhi ya tovuti katika matokeo ya utafutaji.

MakeUseOf mara kwa mara hutoa vidokezi muhimu, kama vile 4 Anonymous Web Browsers That Are Completely Private.

6 Unique & Free Keyword Research Tools You Didn’t Know You Needed, kutoka kwa Search Engine Journal.

This Tool Shows Exposed Cameras Around Your Neighbourhoodmakala katika Motherboard inayoeleza jinsi Kamerka inaweza ikachukua anwani, ishara fulani ardhini, au anwani za kijiografia na kuonesha kamera zilizounganishwa na intaneti na zimeachwa wazi kwenye ramani.

Open-Source Intelligence (OSINT) Reconnaissance, makala ndefu iliyoandikwa na “mtafiti-mwandishi-mdukuzi-mbuni” Ian Barwise katika  Medium, inaangazia mbinu kama vile “Google dorking.”

After the GDPR: researching domain name registrations inaangazia athari za Sheria ya Kulinda Data barani Uropa, inayofanya kutafitia sajili za majina ya kikoa kuwa mgumu, na kwa hiyo kulazimisha matumizi ya vifaa na mbinu tofauti, kwa mujibu wa OSINTCurious.

How to Write Facebook Graph Search Queries mwongozo wa WikiHow  wa 2020 kuhusu matumizi ya sintaksia ya jedwali la utafutaji la Facebook ili kupata machapisho, maoni, watu, na vipengee halisi vinginevyo kwenye Facebook.

The Most Comprehensive TweetDeck Research Guide in Existence (Probably) na Charlotte Godart, mpekuzi na mkufunzi wa Bellingcat (2019).

Finding Hidden Business Resources ni wasilisho la Mary Ellen Bates juu ya kutafuta nyenzo kwenye wavuti wenye kina lililotolewa wakati wa kongamano la Special Libraries Association 2019.

Our Search for the Best OCR Tool, and What We Found, na Ted Han na Amanda Hickman katika Source (2019).

17 Great Search Engines You Can Use Instead of Google, ilichapishwa na Search Engine Journal mwaka 2020.

Instagram Location Search tazama maelezo ya Instagram kuhusu chaguzi za utafutaji nyinginezo.

Makala hii imetafsiriwa na Kabugi Mbae, mwanahabari wa Kenya na mwanachama wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).

Republish our articles for free, online or in print, under a Creative Commons license.

Republish this article


Material from GIJN’s website is generally available for republication under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International license. Images usually are published under a different license, so we advise you to use alternatives or contact us regarding permission. Here are our full terms for republication. You must credit the author, link to the original story, and name GIJN as the first publisher. For any queries or to send us a courtesy republication note, write to hello@gijn.org.