Accessibility Settings

color options

monochrome muted color dark

reading tools

isolation ruler

Ripoti

Miongozo ya Uanahabari wa Upekuzi

Je, unatafuta vidokezi, vifaa na mafunzo? Miongozo ifuatayo inaangazia uanahabari wa upekuzi na inatoa vielelezo na mifano kutoka duniani kote. Mingi ya miongozo haina malipo.

Unaweza pia kupata miongozo hiyo kwa lugha za Kichina na Kihispania. Je, una nyongeza ungependa kuishirikisha wengine? Tutumie barua pepe na kutujulisha.

Uanahabari wa Upekuzi

Modern Investigative Journalism: Na Mark Lee Hunter na Luuk Sengers, wakiwa na Marcus Lindemann. Unaelezewa kama mtaala ambao “unakwenda zaidi ya kile kinachopaswa kufundishwa: unawasaidia wakufunzi wanaoanza kufundisha kwenye tasnia kuona jinsi ya kuifundisha, kwa kuelezea maswali ya kawaida watakayouliza wanafunzi (pamoja na majibu), pamoja na mazoezi ya darasani na kazi za ziada zinazotoa mafunzo kupitia mjadala wa ubunifu na uzoefu.” Umeandikwa na waandishi wa Story-Based Inquiry (tazama hapo chini). Tazama pia slaidi kutoka kwa wasilisho la GIJC19.

Investigative Journalism Manual: Mwongozo huu muhimu ulianza kama kijitabu cha maelezo kwa wanahabari wa Afrika, ukiwa na vielelezo na mifano, uliochapishwa na wakfu wa Kijerumani, Konrad Adenauer Stiftung. Tolea la karibuni zaidi ni la dunia yote na linawalenga wanahabari wanaokabiliwa na sheria kandamizi kwa vyombo vya habari, ukosefu wa uwazi, na uhaba wa rasilimali. Unapatikana pia katika Bahasa na Kimongolia, na kama tovuti ya maingiliano.

Digging Deeper: A Guide for Investigative Journalists in the BalkansHuu ni mwongozo uliochapishwa na BIRN na unapatikana kwa ununuzi. BIRN, kifupi cha Balkan Investigative Reporting Network, huangazia jinsi ya kuchimbua rekodi na data katika eneo hilo. Mwandishi Sheila Coronel ambaye ni mkurugenzi wa Stabile Center for Investigative Journalism, katika chuo kikuu cha Columbia pia anatoa vidokezi na mbinu kuhusu uanahabari wa upekuzi. Pakua sura ya kwanza bila malipo. LughaKiingerezaKimakedonia.

Drehbuch der Recherche (Mswada wa Uchunguzi). Na Mark Lee Hunter na Luuk Sengers, umechapishwa kwa Kijerumani na Netzwerk Recherche. Lugha: Kijerumani

Exposing the Truth: A Guide to Investigative Reporting in AlbaniaMwongozo huu wenye kurasa 73 unajumuisha vielelezo, vidokezi na mbinu zilizohakikiwa. Umechapishwa na OSCE na Balkan Investigative Reporting Network. Lugha: KialbaniaKiingereza.

The Hidden Scenario, ni kitabu cha 2019 kilichoandikwa na Luuk Sengers na Mark Lee Hunter.Kinaangazia jinsi ya kuunda taswira inayoweza kukusaidia kuchunguza.” Kinapatikana kwa ununuzi kutoka kwa Center for Investigative Journalism.

Follow the Money: A Digital Guide to Tracking CorruptionKijitabu hiki cha maelezo kinapatikana bila malipo na kimechapishwa na International Center for Journalists. LughaKiingerezaKirusi, Kigeorgia

Global Investigative Journalism CasebookKitabu hiki kinaambatisha Story-Based Inquiry (tazama hapo chini). Kinajumulisha makala ya upekuzi pamoja na taarifa za msingi kuhusu jinsi wanahabari walivyotafiti na kuandika makala zao. Lugha: Kiingereza

Global Investigative Journalism: Strategies for Support:  Ni utafiti na mjadala wa ueneaji duniani wa uanahabari wa upekuzi ulioandikwa na David E. Kaplan wa GIJN. Unajumuisha vidokezi kuhusu muundo wa mashirika ya upekuzi yasiyo ya faida na vyanzo vya ufadhili wa kifedha, pamoja na mwongozo kwa makundi mbali mbali ulimwenguni kote. Umechapishwa na Center for International Media Assistance. Lugha: Kiingereza

Citizen Investigation Guide Mwongozo huu wa mwaka 2019 kutoka kwa GIJN unanuia kuwasaidia wananchi kuhusika kwenye uanahabari wa upekuzi.

Guide to Investigative Journalism: Mfululizo huu mwepesi uliofanywa na Public Broadcasting Service nchini Marekani unamwongoza mwanahabari katika jinsi ya kutambua makala ya kupekua, kufanya mahojiano ya upekuzi, kugundua stakabadhi ziliko na hatimaye kuzipata, kufanya makala yenyewe, na kuiwasilisha kwa umma. Lugha: Kiingereza

Hidden Scenario, na Luuk Sengers and Mark Lee Hunter [Unapatikana kwa ununuzi kutoka kwa Centre for Investigative Journalism]. Unaonyesha jinsi mbinu za uwasilishaji wa taarifa zinaweza kuupa uanahabari wa upekuzi muundo na uzingatifu. Lugha: Kingereza.

Introduction to Investigative Reporting, na Brant Houston (Poynter News University). Kozi hii ya mtu kujielekeza mwenyewe inagharimu dola za Marekani 29.95 (US$29.95).

Investigating Religion: An Investigative Reporter’s Guidena Debra L. Mason na Amy B. White [unapatikana kwa ununuzi kutoka kwa IRE]Lugha: Kiingereza

Investigative Journalism ManualMwongozo huu mpana uliochapishwa na Forum for African Investigative Reporters (FAIR), unatoa ukwasi wa vidokezi, zikiwemo sehemu mahususi kuhusu afya na maadili, na vielelezo kutoka barani Afrika. LughaKiingerezaKifaransaKireno

Investigative Journalist’s Guide to Company Accounts na Raj Bairoliya. Mwongozo huu uliochapishwa na Centre for Investigative Journalism na unaopatikana kwa ununuzi unawalenga wanahabari wapekuzi wanaohitaji kuelewa mahesabu ya kampuni (hasa kampuni za biashara) au kupata uelewa wa biashara ili kuuliza maswali “yalio sahihi”.

Investigative Online SearchMwongozo huu uliochapishwa mwaka 2011 na shirika la Centre for Investigative Journalism lenye makao yake Uingereza, unajadili jinsi ya kupata taarifa mtandaoni na kuthibitisha ukweli wake. Lugha: Kiingereza

 Investigative Photography: Supporting a Story with Pictures, na CJ Clarke, Damien Spleeters, na Juliet Ferguson [unapatikana kwa ununuzi kutoka kwa Centre for Investigative Journalism]Lugha: Kiingereza

Investigative Reporter’s Handbook, Toleo la 5, na Brant Houston na Investigative Reporters and Editors. Mwongozo huu wa pekee kuhusu jinsi ya kuchunguza kashfa zinazowahusu watu mashuhuri unapatikana kwa ununuzi kutoka kwa IRELugha: Kiingereza

Investigative Reporting: A Toolkit for Reporters: Huu ni mwongozo wa kurasa 107 uliochapishwa mwaka 2009 na US Center for International Private Enterprise na kufadhiliwa na USAID na Al-Masry Al-Youm for Journalism and Publication. Lugha: Kiingereza

Investigative Reporting in Emerging Democracies: Models, Challenges, and Lessons Learned: Hii ni ripoti iliyoandikwa na Drew Sullivan wa Organized Crime and Corruption Reporting Project, yenye vidokezi kuhusu uundaji wa programu, udumishaji wa vigezo, hitaji la wahariri, usalama na kadhalika. Umechapishwa na Center for International Media Assistance. Lugha: Kiingereza

Manual for Arab Journalists on Freedom of Information and Investigative Reporting: Kijitabu hiki chenye kurasa 21 kiliandikwa na Article 19 na kufadhiliwa na United Nations Development Programme. Kinaweza kupakuliwa mtandaoni bila malipo. Lugha: KiingerezaKiarabu

The News Initiative ni mwongozo wa Google unaotoa kozi yenye vipengee tisa kuhusu uanahabari wa upekuzi na unaelekeza katika matumizi ya vifaa vya Google.

The Science Writers’ Investigative Reporting Handbook ni kitabu cha Liz Gross cha mwaka 2018 kuhusu jinsi ya kuchunguza kiini cha makala kilichofanywa kutambua upendeleo, na kupata habari iliyofichwa.

Raising Hell: A Citizen’s Guide to the Fine Art of Investigation (PDF): Center for Investigative Reporting, kituo cha kwanza cha uanahabari wa upekuzi kisicho cha faida duniani, kinatoa mwongozo huu ili kuufundisha umma jinsi ya “kuchunguza, kufichua ufisadi, na kuweka wazi sehemu dhaifu za mamlaka” Lugha: Kiingereza

Recherche in der Praxis: Informanten zum Reden bringen, Fakten hart machen, Missstände aufdecken (Research in Practice: Get Informants to Talk, Get Hard Facts, and Uncover Abuses na Catherine Boss na Dominique Strebel [unapatikana kwa ununuzi]. Lugha: Kijerumani

Reporting in Indigenous Communities uliandikwa na mwanahabari wa Canadian Broadcasting Corporation Duncan McCue mwaka 2011. Unaweza ukatumiwa kuangazia kimataifa watu asilia. Tazama mambo ya kuzingatia aliyoandika McClue, blogu yake na mahojiano naye ya mwaka 2018.

Story-Based Inquiry: Mwongozo mpana kuhusu uanahabari wa upekuzi ulioandikwa kwa ushirikiano na Mark Hunter, Drew Sullivan, Pia Thosden, Rana Sabbagh na Luuk Sengers. Mwongozo huu uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unatumia vielelezo kuelezea mbinu na ujuzi ikiwemo utafiti uandishi, udhibiti wa ubora, na usambazaji. LughaKiingereza (PDF); Kiarabu | العربية (PDF); Kichina  | 中文 (PDF); Kifaransa | Français (PDF); Kirusi | русский (PDF); Kireno | Português (PDF); Kihispania | Español (PDF).

The Story Tells the Facts, na Mark Lee Hunter and Luuk Sengers, [unapatikana kwa ununuzi kutoka kwa Centre for Investigative Journalism]. Unaonyesha mbinu za simulizi, ikiwemo jinsi ya kufanya makala inayopiga kwa nguvu na kwa haraka, na inayoelekea kwenye tamati iliyo na mnato. Lugha: Kiingereza

Undercover Reporting sio mwongozo bali ni hifadhidata ya mtandaoni na kituo cha rasilimali kilichotokana na utafiti uliofanywa kwa ajili ya kitabu Undercover Reporting: The Truth About Deception.  Tovuti hii inachukua mifano mingi ya kipindi cha zaidi ya miaka 100 iliyopita.

The Verification Guide for Investigative Journalists uko na sura 10 na vielelezo vitatu. Mada zake zinajumuisha vifaa vya kutafiti mtandaoni, data, matini zinazotokana na watumiaji na maadili. Ni mwenzi wa The Verification Handbook na Verification Handbook: Additional Materials. Bofya hapa ili kupakua au kununua, na kutazama matoleo yaliyotafsiriwa.

A Watchdog’s Guide to Investigative Reporting: Unasisitizia uanahabari barani Afrika. Mwongozo huu wa mwaka 2005 kwa lugha ya Kiingereza “unatoa mifano ya utendakazi bora na unaangazia changamoto za tasnia hii kwa wale wenye shauku ya kufanya kazi za upekuzi.”

Uanahabari wa Data

Lessons from 30 Years Of Teaching Journalists Data Journalism, ni jarida la GIJC19 lilioandikwa na Brant Houston, mwenyekiti wa Knight kwenye Uanahabari wa Upekuzi katika chuo kikuu cha Illinois. Kwa zaidi ya mwongo mmoja, alikuwa mkurugenzi mkuu wa Investigative Reporters and Editors.

Teach Computational Thinking, Not Just Spreadsheets or Coding, ni jarida la GIJC19 lilioandikwa na Paul Bradshaw, chuo kikuu cha Birmingham City/Kitengo cha Data cha BBC.

7 countries, 9 teachers: a dossier of data journalism teaching strategies Ni njia gani zenye ufanisi za kuwatambulisha wanafunzi kwa data? Na Nouha Belaid, Anastasia Valeeva, Bahareh Heravi, Roselyn Du, Kayt Davies, Adrian Pino, Eduard Martín Borregon, Soledad Arreguez, na Jeff Kelly Lowenstein.

Data and Computational Journalism, makala hii ya mwaka 2020 “inatoa mapendekezo manne yatakayowasaidia wakufunzi kurekebisha mitaala ili kuupa nafasi ujumuishaji wa data katika uanahabari ambao unafanyika upesi.” Waandishi ni Norman P. Lewis, Mindy McAdams, na Florian Stalph. Zifuatazo ni hoja nne zao:

Mosi, maagizo katika hesabu na maelezo ya msingi kuhusu takwimu lazima yahitajike aidha kama moduli katika kozi zilizopo au kama masomo ya kando. Pili, wanafunzi wanapaswa kufunzwa kujiepusha na makosa ya kufasili na uandishi kuhusu data kwenye madarasa ya uanahabari na ya taswira. Tatu, kozi za maadili zinapaswa kujadili data kama kifaa cha uwazi kinacholeta mitanziko tofauti. Nne, uhalisia wa kufikiri kama wanasayansi wa kompyuta, au jinsi ya kuchambua na kutatua matatizo kama ifanyavyo kompyuta, vinaweza kujumuishwa kwenye madarasa yaliyopo yanayofundisha mantiki.

More Effective Teaching of Data Journalism to Working Journalists, na Kuang Keng Kuek Ser wa Data-N, uliowasilishwa katika GIJC19. Vidokezi hivi vinawalenga wakufunzi/walimu wanaofundisha uanahabari wa data kwa wanahabari ambao ni wapya kwenye tasnia hii.

Hacking the curriculum: How to teach data reporting in journalism schools hii ni ripoti ya American Press Institute ya mwaka 2018. “Pendekezo letu kuu ni kuwa vyuo vya uanahabari vichukulie data na hesabu kama ujuzi wa msingi kwa wanafunzi wote.”

Where in the world can I study data journalism? Makala hii ya mwaka 2019 iliyoandikwa na Bahareh Heravi inatoa muhtasari wa nakala yake ya kiakademia kuhusu mada ya uanahabari wa data kwa jina 3Ws of Data Journalism Education, iliyochapishwa na Data Journalism Practice. Nakala hii inaweza patikana katika UCD academic repository. Inajumuisha ramani.

International Journalism Education Consortium: Hizi ni linki na maelezo ya mitaala ya kozi za uanahabari wa data na zinazofundishwa kupitia usaidizi wa kompyuta. (Inafuata mpangilio wa abjadi ya chuo kikuu, kisha jina la profesa)

Computer-Assisted Reporting: A Comprehensive Primer: Na Fred Vallance-Jones na David McKie [inapatikana kwa ununuzi]. Lugha: Kiingereza

Computer-Assisted Reporting: A Practical GuideToleo la nne na Brant Houston [linapatikana kwa ununuzi]. Lugha: Kiingereza

Computer-Assisted Research: Information Strategies and Tools for JournalistsNa Nora Paul na Kathleen A. Hansen [unapatikana kwa ununuzi kutoka IRE]. Lugha: Kiingereza

Data Journalism Handbook ni juhudi ya ushirikiano wa kimataifa inayohusisha watalaamu wengi wa uanahabari wa data. Inajumuisha maelezo, vielelezo, na vidokezi kuhusu jinsi ya kupata, kutumia na kuchanganua data. Ni mradi wa European Journalism Centre na Open Knowledge Foundation. Lugha: Inaweza ikapakuliwa mtandaoni kwa KiarabuKiingerezaKifaransaKirusi, na Kihispania. Kijitabu hiki pia kimetafsiriwa kwa lugha nyinginezo, ikiwemo Kigeorgia. Toleo la 2012 lilitafsiriwa kwa zaidi ya lugha 12 — ikiwemo Kiarabu, Kichina, Kicheki, Kifaransa, Kigeorgia, Kigiriki, Kiitalia, Kimakedonia, Kireno, Kirusi, Kihispania na Kiukraine.

Flowing Data inasimamiwa na mtakwimu Nathan Yau, ambaye ni mwandishi wa Data Points: Visualization that Means Something na Visualize This: The FlowingData Guide to Design, Visualization, and Statistics. Sehemu ya Learning to Data ina linki za mafunzo, vitabu na miongozo inayohusiana na utendakazi kwa data.

Mapping for Stories: A Computer-Assisted Reporting Guide, Na Jennifer LaFleur na Andy Lehren [inapatikana kwa ununuzi kutoka kwa IRE]. Lugha: Kiingereza

Precision Journalism: a Reporter’s Introduction to Social Science Methods, Na Philip Meyer [inapatikana kwa ununuzi]. Lugha: Kiingereza

Datawrapper ni nyenzo za kuendeshea semina.

Kwa habari zaidi kuhusu rasilimali za jumla za uanahabari wa data, tazama ukurasa wetu wa Data Journalism Resource.

Ufundishaji na Mazoezi

Model Curricula for Journalism Education: Huu ni mwongozo unaolenga kitivo cha uanahabari katika nchi zinazoendelea na demokrasia zinazoibuka. Mwongozo huu ulioundwa na UNESCO unatoa mitaala ya kozi 17 – ukiwemo uanahabari wa upekuzi – ambayo yaweza ikatumika kukidhi mahitaji ya kila nchi. Lugha: Kiingereza (PDF); Kifaransa | Français (PDF); Kihispania | Español (PDF); Kirusi | Pусский (PDF); Kiarabu | العربية (PDF); Kichina | 中文 (PDF); Kinepali (PDF); Kireno | Português (PDF); Kiajemi | فارسی (PDF).

International Journalism Education Consortium: Ni maelezo ya kozi na mitaala ya uanahabari wa upekuzi kutoka kwa kozi za uanahabari wa upekuzi. (Inafuata mpangilio wa abjadi ya chuo kikuu, kisha jina la profesa)

The James W. Foley Journalist Safety Guide: A Curriculum Plan For College Journalism and Communications Instructors Ni mipango yenye kina ya kozi ya vipindi vitano, ambayo inajenga kwa sehemu, juu ya makala ya HBO kuhusu James Foley, mwanahabari aliyeuawa Agosti 19, 2014, nchini Syria. Mtaala wenyewe unajumuisha nyenzo za marejeleo, hasa makala za wanahabari wanaofanya kazi katika hali za hatari. Matukio yameelezewa pamoja na maswali ya mijadala. Unaweza ukaupata mtaala huo ukitumia nywila “FoleySafety”.

Algorithms for Journalists: Ni mtaala wa kozi ya darasa la algorithimu linalofundishwa na mwanahabari na mwanasayansi wa kompyuta Jonathan Stray kwenye programu ya The Lede katika Chuo cha Uanahabari cha Columbia. Unapatikana katika GitHub, pamoja na linki za slaidi, nyenzo ya kusoma na mazoezi. Zingatia kuwa darasa hili linawalenga wanafunzi ambao wana kiwango cha mwanzoni cha uundaji programu kwa kutumia lugha ya kompyuta ya Python.

Better News Tovuti yenye rasilmali nyingi inayoendeshwa na American Press Institute.

AEJMC Task Force for Bridges to the Professions 2017 Report Ni ripoti ya mwaka 2017 juu ya ushirikiano baina ya akademia na wanahabari kutoka kwa Muungano wa Elimu katika Uanahabari na Mawasiliano ya Umma (AEJMC).

Observations on how we teach drone journalism, na Judd Slivka, mkurugenzi wa kwanza wa uandishi wa habari kupitia ndege zisizo na rubani katika Chuo cha Uanahabari cha Missouri.

Algorithms course materials at Columbia Journalism School  Ni mtaala wa kufundishia algorithimu uliotayarishwa na profesa Jonathan Stray wa chuo kikuu cha Columbia.

The Field Guide to Security Training ni mtaala ambao mwenyeji wake ni OpenNews, timu inayowasaidia wasanidi programu, wabuni, na wachanganuzi wa data kukutana na kushirikiana kwenye miradi ya uanahabari unaoshirikisha michango ya yote, na BuzzFeed Open Lab, programu ya usomi wa Sanaa na teknolojia katika BuzzFeed News.

Dig Deep & Aim HighHuu ni mwongozo uliochapishwa na International Center for Journalists mwaka 2000 kuhusu jinsi ya kufundisha mbinu za upekuzi. Lugha: Kiingereza.

Miongozi Mingine Muhimu

Empowering Independent Media: U.S. Efforts to Foster a Free Press and an Open Internet Around the World: Ni mtazamo mpana kuhusu maendeleo ya vyombo vya habari ambao unavifaa vyombo vya habari visivyo vya faida na mashirika yasiyo ya serikali katika mataifa yanayoendelea na yaliyo kwenye mpito. Unaangazia sehemu saba kuu za maendeleo ya vyombo vya habari: ufadhili, vyombo vya habari vya kidijitali, uendelevu, sheria ya vyombo vya habari, usalama, elimu, ufuatiliaji na tathmini. Lugha: KiingerezaKihispaniaKifaransa.

Google Search Tips for Journalists: Mwongozo huu mfupi na wa msaada unatoa vidokezi muhimu vya kutafiti kwa ufanisi zaidi kupitia huduma ya Google Search. Umekusanywa na Expertisefinder.com.

Journalist Survival Guide: Mwongozo huu wa uhaishaji kimsingi umetengenezwa na Samir Kassir Foundation, wakfu ulioko jijini Beirut, ili kuwasaidia wanahabari na wanaharakati wanaofanya kazi katika maeneo yenye vita na migogoro. Pia unajumuisha vidokezi kuhusu usalama wa kidijitali na jinsi ya kuziba nyayo zako mtandaoni. Lugha: KiingerezaKiarabu.

Legal Leaks Toolkit: A Guide for Journalists on How To Access Government Information: Ni kijitabu muhimu chenye kurasa 75 kinachoangazia mambo ya msingi kwa wanahabari wanaotumia taratibu rasmi ili kupata habari rasmi. Kimeandaliwa na Access Info Europe na Network for Reporting on Eastern Europe n-ost. Kinapatikana kwa KiingerezaKiitalia, na lugha nane za kanda ya Mashariki mwa Uropa.

Reporting Atrocities: A Toolbox for Journalists Covering Violent Conflict and Atrocities: Mwongozo huu wa kina wenye kurasa 61 unaangazia asili ya mgogoro, namna ya kuripoti kuuhusu, na wajibu wa mwanahabari katika hali kama hizo. Umeandikwa na mwanahabari wa Afrika Kusini Peter du Toit na kuchapishwa na Internews. Lugha: Kiingereza.

Reporting on Corruption: A Resource Tool for
Governments and JournalistsMwongozo huu wenye kurasa 117 uliotengezwa na Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Matumizi ya Dawa na Uhalifu (UNODC) unazamia mijadala ya urasimu na maongezi kuhusu Umoja wa mataifa, lakini una rasilimali na vielelezo muhimu. Unajumuisha ulinzi kwa vyanzo vya habari, haki ya kupata habari, na mbinu za kujisimamia.

SEEMO Safety Net Manual: Guidelines for Journalists in Extraordinary or Emergency Situations: Mwongozo huu kuhusu usalama uliochapishwa na South East Europe Media Organization–ni sehemu ya mpango mpana wa kuwalinda wafanyakazi wa vyombo vya habari katika eneo hili. Lugha: Kiingereza na, mtu akituma ombi, kwa lugha za Kiserbia, Kiitalia, Kiromania, Kigiriki, Kituruki, Kibulgaria, Kikroatia, na Kisloveni.

Tragedies & JournalistsMwongozo huu wenye kurasa 40-page una vidokezi vya kutendea vinavyolenga kuwasaidia wanahabari, wanahabari wa picha, na wahariri wanaporipoti kuhusu dhuluma huku wakiwalinda waathiriwa na wao wenyewe. Ulichapishwa na Dart Center for Journalism & Trauma, na kuandikwa na Joe Hight na Frank Smyth. Lugha: KiingerezaKihispania中文 (Kichina).

Verification Handbook ni rasilimali kwa wanahabari na watoaji msaada inayotoka kwa European Journalism Centre. Inatoa vifaa, mbinu na miongozo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kukabili matini zinazotokana na watumiaji wakati wa dharura. Lugha: KiingerezaKireno العربية , Kihispania.

Who’s Running the Company: A Guide to Reporting on Corporate Governance: Ni utangulizi kwa uanahabari kuhusu utawala wa mashirika, na unajumuisha sehemu juu ya bodi za wakurugenzi, ripoti kuhusu fedha, na ufuatiliaji wa utendakazi wa kampuni. Umetengezwa na taasisi ya International Finance Corporation ya Benki ya Dunia na International Center for Journalists. Lugha: Kiingereza (PDF); Kifaransa | Français (PDF); Kihispania | Español (PDF); Bahasa Indonesia (PDF); Kimongolia | МОНГОЛ ХЭЛ (PDF); Kiarabu | العربية (PDF); Kirusi | Pусский (PDF); and Kireno | Português (PDF).

Security and Covering Conflict: IJNet limekusanya orodha ya miongozo kwa wanahabari wanaoripoti kuhusu usalama na migogoro kutoka kwa mashirika mbalimbali. Baadhi ya miongozo inapatikana kwa lugha kadha zikiwemo Kiarabu, Kichina, Kirusi na Kihispania.

Kihispania Pekee

Ifuatayo ni miongozo inayopatikana kwa Kihispania pekee. Tazama pia ripoti zilizoorodheshwa hapo huu – nyingi yazo zimechapishwa kwa Kihispania – na vilevile ukurasa huu wa rasilimali kwa Kihispania.

Cómo Investigar Temas Ambientales (Investigating Environmental Issues): Huu ni mwongozo wa kuchunguzia masuala ya mazingira katika Marekani ya Kusini.

Guía Práctica sobre Periodismo de Datos (Practical Guide to Data Journalism) na Sandra Crucianelli, msomi wa Knight International Journalism. Mwongozo huu unatoa vidokezi kuhusu uundaji wa taswira ya data na unaangazia vielelezo vya wanahabari wanaohusika na uanahabari wa data. Umechapishwa na International Center for Journalists.

Manual de Periodismo de Datos Iberoamericano (Latin American Handbook of Data Journalism) unatoa vidokezi na mafunzo kuhusu kuchimba data, kutafiti kwa kina mtandaoni, uundaji wa taswira ya data, na kadhalika. Mwongozo kwa wanahabari wanaozungumza Kihispania umechapishwa na Poderomedia Foundation kwa ushirikiano na Chuo cha Uanahabari katika University Alberto Hurtado.

Métodos de la Impertinencia (Methods of Impertinence)Tawi la Press and Society Institute (IPYS) nchini Venezuela lilitoa mkusanyiko wa mbinu bora na masomo ya uanahabari wa upekuzi katika Marekani ya Kilatini. Kitabu hiki kinajumuisha shuhuda kutoka kwa wanahabari maarufu katika eneo hilo.

Periodismo de Investigacion (Investigative Journalism) na Gerardo Reyes. Ni mwongozo mpana kuhusu uanahabari wa upekuzi katika Marekani ya Kilatini unaojumuisha sehemu kuhusu mikakati na mbinu.

Periodista de Investigacion Latinoamericano en la Era Digital (The Latin American Journalist: Research in the Digital Age) umetengezwa na Initiative for Journalism Research in the Americas na ICFJ kwa ushirikiano na Connectas. Umeandikwa kwa pamoja na Nathalia Salamanca, Jorge Luis Sierra, na Carlos Eduardo Huertas.

Makala hii imetafsiriwa na Kabugi Mbae, mwanahabari wa Kenya na mwanachama wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).

Republish our articles for free, online or in print, under a Creative Commons license.

Republish this article


Material from GIJN’s website is generally available for republication under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International license. Images usually are published under a different license, so we advise you to use alternatives or contact us regarding permission. Here are our full terms for republication. You must credit the author, link to the original story, and name GIJN as the first publisher. For any queries or to send us a courtesy republication note, write to hello@gijn.org.