Accessibility Settings

color options

monochrome muted color dark

reading tools

isolation ruler

GIJN Africa: Kupata Rekodi za Umma

Katika mataifa mengi ya kusini mwa jangwa la Sahara, kupata habari za umma ni jinamizi mpaka leo. Hii ni kwa sababu hakuna sheria zinazofadhili maombi ya kupata rekodi za wanahabari, au zinazowashinikiza maafisa wa serikali kusalimisha rekodi za umma zinazomilikiwa na serikali.

Hata hivyo, baadhi ya mataifa yamebadili mkondo na kurahisisha mchakato wa kupata habari za umma. Zifuatazo ni baadhi ya rasilimali bora zaidi kwa wanahabari wa kusini mwa jangwa la Sahara watafutao habari za umma katika mataifa yaliyo na sheria zinazodhibiti upatikanaji wa habari.

Africa Freedom of Information Centre ni mojawapo ya rasilimali pekee zinazoangazia bara la Africa. Hutoa habari kuhusu sheria za Uhuru wa Kupata Habari (FOI) barani Afrika.

IFEX linatoa maelezo mazuri juu ya upanuzi wa sheria za Uhuru wa Kupata Habari barani Afrika, yakiwemo baadhi ya matatizo yanayojitokeza katika utekelezaji wake.

Kenya: Reporting on Good Governance in Kenya.org linaelezea sheria za kitaifa na za majimbo, na kanuni za kupata habari. Vilevile huwa linachapisha ripoti kuhusu uzoefu wa wanahabari na picha za taswira zenye mnato. Pia tazama kijitabu cha maelezo kuhusu sheria ya Kenya kilichotengenezwa na Katiba Institute.

Liberia: InfoLib hutoa utaratibu wa mtandaoni ili kufadhili maombi ya kupata habari kupitia sheria ya Uhuru wa Kupata Habari. Ijapokuwa ni huduma inayoendeshwa kwa kujitegemea, inaweza patikana chini ya kichupo cha “Take Action” kwenye tovuti ya tume ya habari ya Liberia.

Mozambique: Guia do Direito à Informação Para Jornalistas, ni mwongozo wa mwaka 2016 kuhusu Uhuru wa Kupata Habari kwa wanahabari ulioandaliwa na IREX.

Nigeria: R2KNigeria hutoa habari thabiti kuhusu sheria ya Uhuru wa Kupata Habari. Idara ya Nigeria Extractive Industries Transparency Initiative ina jukwaa la Uhuru wa Kupata Habari linalofadhili utumaji wa maombi mtandaoni. Nayo idara ya Bureau of Public Service Reforms vile vile ina jukwaa la Uhuru wa Kupata Habari. Mradi wa Haki za Kijamii na Uchumi na Uwajibikaji mnamo Aprili 2018 ulichapisha mwongozo: Kutumia haki yako ya kupata habari kupinga ufisadi katika sekta za afya, elimu na maji.

Rwanda: Sobanukirwa ni tovuti isiyo na malipo inayofadhili maombi ya kupata habari. Inapatikana kwa lugha za KiingerezaKinyarwanda au Kifaransa.

South Africa: Open Democracy Advice Centre (ODAC) hutoa fomu za kuomba stakabadhi kupitia Sheria inayohamasisha Upatikanaji wa Habari (Promotion of Access to Information Act), na pia usaidizi. Right2Know ni kundi muhimu la uhamasishaji wa uwazi. ODAC hutoa usaidizi juu ya haki ya kupata habari ambayo inapatikana katika Hamasisho la Upatikanaji wa Habari.

Media Institute of Southern Africa pia ina ukurasa wenye linki zinazoelekeza kwenye sheria za Uhuru wa Kupata Habari za Afrika.

Uganda: Ask your Gov Uganda ni jukwaa la mtandaoni la kuwasilishia maombi ya kupata habari kupitia Uhuru wa Kupata Habari. Watumiaji wa jukwaa hili wanaweza kutuma maombi ya kupata habari moja kwa moja kwa taasisi za serikali. Tovuti hii pia huchapisha hadharani majibu ya maombi yaliyotumwa.

Makala hii imetafsiriwa na Kabugi Mbae, mwanahabari wa Kenya na mwanachama wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).