{"id":281150,"date":"2014-07-16T15:46:40","date_gmt":"2014-07-16T19:46:40","guid":{"rendered":"https:\/\/gijn.org\/?page_id=281150"},"modified":"2023-06-28T11:39:14","modified_gmt":"2023-06-28T15:39:14","slug":"uanahabari-wa-upekuzi-jinsi-ya-kuielezea-sanaa-hii","status":"publish","type":"page","link":"https:\/\/gijn.org\/sw\/kuhusu-sisi\/uanahabari-wa-upekuzi-jinsi-ya-kuielezea-sanaa-hii\/","title":{"rendered":"Uanahabari wa Upekuzi: Jinsi ya Kuielezea Sanaa Hii"},"content":{"rendered":"<p><a href=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/03\/gijnafricaheader-1.png\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" class=\"aligncenter wp-image-223911 size-full\" src=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/03\/gijnafricaheader-1.png\" alt=\"\" width=\"770\" height=\"187\" srcset=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/03\/gijnafricaheader-1.png 770w, https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/03\/gijnafricaheader-1-336x82.png 336w, https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/03\/gijnafricaheader-1-768x187.png 768w\" sizes=\"auto, (max-width: 770px) 100vw, 770px\" \/><\/a><\/p>\n<p>Ijapokuwa maelezo ya uanahabari wa upekuzi hutofautiana, kuna makubaliano mapana miongoni mwa makundi ya kitaaluma ya uanahabari kuhusu nguzo zake muhimu: hufuata mfumo maalum, huwa na kina, hutegemea utafiti asilia na uandishi wa habari ambao mara nyingi huhusisha ufichuzi wa siri. Kwa wengine, upekuzi aghalabu huhusisha matumizi mengi ya data na rekodi za taarifa za umma, huku ukiangazia haki ya kijamii na uwajibikaji.<a href=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Defining-IJ.jpg\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" class=\"alignright wp-image-281151 size-full\" src=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Defining-IJ.jpg\" alt=\"\" width=\"179\" height=\"179\" srcset=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Defining-IJ.jpg 179w, https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Defining-IJ-140x140.jpg 140w, https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/Defining-IJ-60x60.jpg 60w\" sizes=\"auto, (max-width: 179px) 100vw, 179px\" \/><\/a><\/p>\n<p><a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"http:\/\/unesdoc.unesco.org\/images\/0019\/001930\/193078e.pdf#193103\">Kanuni ya Uanahabari wa Upekuzi<\/a> iliyochapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inaeleza hivi: \u201cUanahabari wa upekuzi huhusisha kuufichulia umma mambo yaliyofichwa aidha makusudi na mtu aliye na mamlaka, au yaliyofichwa bila kukusudia kwenye mlundikano wa taarifa nyingi au mazingira yanayozuia uelewa wa watu. Hutegemea matumizi ya stakabadhi na vyanzo bayana na vya siri.\u201d Kikundi kimoja cha wanahabari wapekuzi kinachotumia lugha ya Dutch na Flemish kwa jina VVOJ kinaelezea uanahabari wa upekuzi kwa mkato: <a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"https:\/\/www.vvoj.org\/2009\/01\/11\/investigative-journalism-in-europe-part-1-introduction\/\">\u201cni uanahabari changanuzi na wenye kina.\u201d<\/a><\/p>\n<aside class=\"module align-right half type-pull-quote\"><em>Kupata video yetu ambatanishi,\u201cUanahabari wa Upekuzi ni Nini\u201d, tazama <\/em><a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"https:\/\/www.youtube.com\/watch?v=TCVU52T6Cbs\"><em>mtandao wa GIJN wa YouTube.<\/em><\/a><\/aside>\n<p>Baadhi ya wanahabari, kwa hakika, wanadai kuwa kwa jumla uandishi wa habari ni uanahabari wa upekuzi. Kuna ukweli fulani katika madai haya \u2013 mbinu za upekuzi hutumiwa pakubwa na wanahabari ambao huangazia nyanja maalum huku wakiripoti ndani ya muda waliopewa, na vile vile na washiriki wa \u201ckikosi cha upekuzi\u201d walio na wiki kadha za kushughulikia makala fulani. Lakini uanahabari wa upekuzi ni mpana kuliko hivi \u2013 ni mkusanyiko wa mbinu ambazo ni sanaa inayoweza kumchukua mtu miaka mingi kuielewa kwa ustadi. Vigezo vya juu vya utafiti na uwasilishaji wa taarifa katika tasnia ya uanahabari wa upekuzi vinathibitishwa na <a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"http:\/\/www.ire.org\/awards\/\">makala yanayonyakua tuzo za juu<\/a>. Tasnia yenyewe huwa na azimio hili: udadisi wa kina unaofuatilia kwa makini sana wizi wa fedha za umma, matumizi mabaya ya mamlaka, uharibifu wa mazingira, kashfa zinazofungamana na afya, na kadhalika.<\/p>\n<aside class=\"module align-right half type-pull-quote\">Kimsingi: Uanahabari wa upekuzi huzingatia mfumo maalum, kina, utafiti asilia na uwasilishaji wa taarifa ambao aghalabu hufichua siri.<\/aside>\n<p>Ingawa wakati mwingine uanahabari wa upekuzi huelezewa kama tasnia, uanahabari wa kina, au unaoripoti kuhusu mradi fulani, hii isieleweke kuwa ni sawa na kile kimekuja kufahamika kwa Kimombo \u201cleak journalism\u201d (uanahabari wa taarifa za siri zitolewazo bila mtoaji kujitambulisha ni nani) \u2013 unahusu taarifa za mara moja anazopata mwanahabari kabla ya wanahabari wengine kupitia stakabadhi au vidokezi vilivyotolewa, kwa kawaida, na watu walio na mamlaka ya kisiasa. Yakini katika demokrasia zinazoibuka, maelezo ya uanahabari wa upekuzi yaweza yasiwe wazi, na makala mara nyingi hutajwa ni ya kipekuzi ikiwa tu yanachanganua au kuhusisha rekodi zilizotolewa pasipo mtoaji kujitambulisha. Makala yanayoangazia uhalifu au ufisadi, uchanganuzi, au hata maoni ya mtu binafsi yanaweza vilevile yakatajwa kimakosa kuwa ni uanahabari wa upekuzi.<\/p>\n<p>Wakufunzi waliobobea wanashikilia kuwa uanahabari wa upekuzi ulio bora zaidi hutumia mbinu yenye umakini huku ukitegemea pakubwa vyanzo vya habari vya msingi, uundaji na ujaribishaji wa makisio, na uhakiki thabiti wa taarifa. <a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"http:\/\/www.merriam-webster.com\/dictionary\/investigation\">Maelezo ya kamusi ya \u201cuchunguzi\u201d<\/a> ni \u201cudadisi wa kimfumo \u201d, ambao kwa kawaida huwezi ukafanyika kwa siku moja au mbili; udadisi wa kina huhitaji muda. Wengine huashiria kwenye mchango wa tasnia hii katika kulimbukisha mbinu mpya, kama vile matumizi yake ya kompyuta kuchanganua data na kuwasilisha taswira yake. \u201cUanahabari wa upekuzi ni muhimu kwa sababu hufundisha mbinu mpya, na njia mpya za kufanya mambo,\u201d alieleza Brant Houston, mwenyekiti wa taasisi ya uanahabari ya Knight katika Chuo Kikuu cha Illinois. Brant aliwahi kuhudumu kwa miaka mingi kama mkurugenzi mkuu wa muungano wa Wanahabari na Wahariri Wapekuzi (Investigative Reporters and Editors). \u201cMbinu hizo hufungamana na uandishi wa habari kila siku. Kwa hiyo, unapandisha vigezo vya taaluma yote.\u201d<\/p>\n<p><em><a href=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/CIMA-Report-336x432-1.png\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" class=\"alignleft wp-image-281152 size-thumbnail\" src=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/CIMA-Report-336x432-1-140x140.png\" alt=\"\" width=\"140\" height=\"140\" srcset=\"https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/CIMA-Report-336x432-1-140x140.png 140w, https:\/\/gijn.org\/wp-content\/uploads\/2020\/10\/CIMA-Report-336x432-1-60x60.png 60w\" sizes=\"auto, (max-width: 140px) 100vw, 140px\" \/><\/a>Makala hii imetolewa kwenye<\/em> <a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"http:\/\/www.cima.ned.org\/publication\/global-investigative-journalism-strategies-for-support\/\"><em>Global Investigative Journalism: Strategies for Support<\/em><\/a><em>, David E. Kaplan, Center for International Media Assistance, 2013. Kaplan ni mkurugenzi mkuu wa Global Investigative Journalism Network, muungano wa makundi 184 yasiyo ya faida katika mataifa 77 ambayo hufanya kazi kufadhili uanahabari wa upekuzi.<\/em><\/p>\n<h5><strong>Mitazamo ya Ziada <\/strong><\/h5>\n<p>Uanahabari wa Upekuzi ni Nini, Sura ya Kwanza kwenye <a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"http:\/\/www.investigative-manual.org\/wp-content\/uploads\/2016\/09\/20171026-IJM_final.pdf\">Mwongozo wa Uanahabari wa Upekuzi<\/a>, ambao ni mradi wa mwaka 2010 wa Global Media Programmes unaoongozwa na Konrad Adenauer Stiftung (KAS).<\/p>\n<p><em>Makala hii imetafsiriwa na\u00a0<a rel=\"noopener\" target=\"_blank\" href=\"https:\/\/twitter.com\/kabugimbae\">Kabugi Mbae<\/a>, mwanahabari wa Kenya na mwanachama wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).<\/em><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Ijapokuwa maelezo ya uanahabari wa upekuzi hutofautiana, kuna makubaliano mapana miongoni mwa makundi ya kitaaluma ya uanahabari kuhusu nguzo zake muhimu: hufuata mfumo maalum, huwa na kina, hutegemea utafiti asilia na uandishi wa habari ambao mara nyingi huhusisha ufichuzi wa siri. Kwa wengine, upekuzi aghalabu huhusisha matumizi mengi ya data na rekodi za taarifa za [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":3031153,"featured_media":0,"parent":1212533,"menu_order":0,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","template":"","meta":{"_acf_changed":false,"_price":"","_stock":"","_tribe_ticket_header":"","_tribe_default_ticket_provider":"","_tribe_ticket_capacity":"","_ticket_start_date":"","_ticket_end_date":"","_tribe_ticket_show_description":"","_tribe_ticket_show_not_going":false,"_tribe_ticket_use_global_stock":"","_tribe_ticket_global_stock_level":"","_global_stock_mode":"","_global_stock_cap":"","_tribe_rsvp_for_event":"","_tribe_ticket_going_count":"","_tribe_ticket_not_going_count":"","_tribe_tickets_list":"[]","_tribe_ticket_has_attendee_info_fields":false,"footnotes":""},"gijn_language":[17800],"gijn_region":[],"class_list":["post-281150","page","type-page","status-publish","hentry","gijn_language-sw-sw"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/281150","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages"}],"about":[{"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/page"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/3031153"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=281150"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/281150\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":1212509,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/281150\/revisions\/1212509"}],"up":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/1212533"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=281150"}],"wp:term":[{"taxonomy":"gijn_language","embeddable":true,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/gijn_language?post=281150"},{"taxonomy":"gijn_region","embeddable":true,"href":"https:\/\/gijn.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/gijn_region?post=281150"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}